TANZIA: Mvumbuzi wa Madini ya Tanzanite afariki dunia
Mzee Jumanne Ngoma ambaye aligundua Madini ya Tanzanite amefariki leo January 30, 2019 ktk Hospital ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma.
Mwaka jana, Rais John Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara alimzawadia Sh.100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini hayo.
from UDAKU SPECIAL BLOG
Comments
Post a Comment