Skendo ya Ushoga na Ubaguzi wa Rangi, zapelekea mkali Empire Jamal, Kudundwa na Wahuni Marekani
Kama unaikumbuka series ya Empire iliyojizolea umaarufu kutokana na waigizaji husika walioshiriki katika series hiyo, Ikumbwe hii ni moja ya series ambayo imeangaliwa sana na kuwapa heshima wakubwa washiriki wa series hiyo.
Na hata siku ya jumatatu mmoja ya washiriki wakubwa wa series hiyo mwanadada Taraji P alimaarufu Cookie Lyon alipewa heshima Hollywood pia akiwa kwenye kipengele cha msanii mwenye hisia, na umaarufu wote amejizolea kutokana series hii.
Sasa siku ya jana ilikuwa mbaya sana kwa mmoja ya washiriki anayejulikana kwa jina la Jussie Smollett alimaarufu Jamal Lyon.
Taarifa zilizotoka jana ziliripoti kuwa, mwigizaji huyo wa Empire alishambuliwa na kupigwa vibaya na wanaume wawili wasiojulikana mjini Chicago kwa sababu za ubaguzi wa rangi pamoja na tuhuma za ‘Ushoga’ yaani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Wanaume hao walimpiga wakati akiingia kwenye mgahawa kupata chakula, walimfunga kamba shingoni na kumpiga vibaya kiasi cha kumvunja mbavu. Walimtolea maneno machafu ya kibaguzi kwa kumwambia hii ni nchi ya watu weupe, yaani “This is MAGA country” msemo wa Rais Donald Trump ambao unapingwa vikali.
Watu maarufu nchini Marekani wameibuka na kupinga vikali vitendo vya ukatili ambavyo amefanyiwa nyota wa filamu Jussie Smollett.
from UDAKU SPECIAL BLOG
Comments
Post a Comment