Majina ya watu 14,200 wanaoishi na virusi vya UKIMWI yavujishwa mtandaoni


Zaidi ya majina 14,000 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini Singapore yamevujishwa mtandaona, hii ni baada ya watu wasiojulikana kudukua taarifa hizo za siri.


Mamlaka za serikali zinazojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama mitandaoni nchini humo, zinaamini aliyehusika na udukuzi huo huenda ni Mmarekani mmoja aliye na virusi vya ukimwi ambaye mpenzi wake alishawahi kuwa daktari wa ngazi ya juu nchini Singapore, hii ni kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC .


Mmarekani huyo, aliyetambulika kwa jina la Mikhy Farrera-Brochez, imeelezwa kuwa alishawahi kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha na dawa za kulevya mwaka 2016.

Mwaka 2017, Mikhy alipimwa na kubainika kuwa ameathirika, lakini taarifa zake mpaka sasa hazipatikani mtandaoni na hajulikani alipo mpaka sasa hivi na serikali inamtafuta.



Mpenzi wa Mikhy, Ler Teck Siang raia wa Singapore ambaye ni daktari mkubwa nchini humo, amekamatwa na vyombo vya dola kwa tuhuma kuwa alimsaidi, Farrera-Brochez kuweka taarifa za uongo katika rekodi zake za matibabu ikiwemo kufuta jina lake mtandaoni.

Waziri wa Afya wa taifa hilo, Gan Kim Jong jana Jumanne Januari 29, 2019 akiongea na Waandishi wa Habari, amesema kuwa walifahamishwa tarehe 22 Januari mwaka huu kuwa majina hayo yaliyovujishwa mtandaoni na wamefanikiwa kuyaondoa.

“Mmoja wa mfanyakazi wetu wa zamani, ambaye alikua na idhini ya kufikia sajili ya taarifa binafsi za watu wenye virusi vya HIV, huenda hakuzingatia mwongozo wa usalama uliyowekwa wa kushughulikia taarifa hizo na kuzilinda,” amesema waziri Yong akimlenga Bi. Siang .

Taarifa za udukuzi zinakuja ikiwa imepita miezi kadhaa, baada ya rekodi za watu milioni 1.5 wa Singapore akiwemo Waziri Mkuu, Lee Hsien Loong kuibiwa mwaka 2019.

Tayari serikali ya Singapore kupitia wizara ya afya, imeomba radhi kufuatia udukuzi huo.

from UDAKU SPECIAL BLOG

Comments

Popular posts from this blog