KIUNGO STAND UNITED AHOJIWA HUKUSU URAIA WAKE
Kiungo wa Stand United Afidh Mussa ambaye inaelezwa uraia wake una utata, amehojiwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga na kutakiwa asiondoke nje ya mkoani huo wakati uchunguzi wa suala lake ukiendelea.
Yanga imepeleka malalamiko TFF ikipinga mchezaji huyo anayedaiwa kuwa raia wa Burundi kusajiliwa na Stand United kama Mtanzania.
Afidh alicheza katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Stand United dhidi ya Yanga uliomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Licha ya kuzaliwa nchini Tanzania, inadaiwa Afidh ana uraia wa Burundi
Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Yanga imenasa vielelezo vinavyothibitisha kiungo huyo kuwa na uraia wa Burundi
Moja ya vielelezo hivyo ni leseni ya mchezaji huyo aliyoitumia mwaka 2017 katika ligi kuu ya Burundi iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini humo likimtambua Afidh kuwa raia wa Burundi
Katika leseni hiyo iliyotolewa Septemba 14 2017, Afidh anatumia jina la Hererimana Afizi Mussa. Ametambulishwa kama raia wa Burundi anayetokea eneo la Cibitoke
Wakati katika klabu ya Stand United kiungo huyo anatambulika kwa jina la Afidh Mussa akiwa amesajiliwa kama Mtanzania leseni yake ikiwa namba 000238M93
Install /Update Application ya Nijuze Habari Uweze Kupata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Comments
Post a Comment