KADETFU NA BUKOBA DC WAINGIA MAKUBALIANO RASMI YA KUFANYA KAZI PAMOJA

 
Anaandika Abdullatif Yunus - Kagera.

Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Kagera Development and Credit Revolving Fund (KADETFU) lenye Makao Makuu yake Manispaa ya Bukoba, limeiingia makubaliano rasmi na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ya kufanya pamoja Shughuli mbalimbali za Kimaendeleo kwa Kushirikiana pande zote mbili.

Hapo awali KADETFU wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kwa ushirikiano mkubwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa Muda mrefu pasina kuwepo Mkataba wa Maelewano, licha ya kuwa shughuli hizo zikiwemo za Kijamii zimekuwa zikifanikiwa kwa kiwango Kikubwa kama yalivyo matarajio yao.

Miongoni mwa shughuli zilizotekelezwa na KADETFU kwa kushirikiana na Halmashauri ya Bukoba ni pamoja na Kujengeana uwezo Kati ya Wataalamu wa pande zote mbili (KADETFU na Halmashauri), kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali, kusaidiana katika shughuli za Kazi, Kuwajengea wananchi uwezo katika masuala ya mipango na bajeti, Masuala ya Upashanaji Habari, Ununuzi wa mashine ya Kusaga iliyopo katika Kata ya Rubale, ununuzi wa Injini ya gari la Halmashauri, kuibua miradi n.k

Hata hivyo kwa Mkataba waliokabidhiana Januari 30, 2019 mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Madiwani, una lenga kuendelea kushirikiana kwa pande zote mbili katika Miradi ya Utawala Bora na Uwajibikaji, kujenga uwezo kwa Kamati za Kata kwa kutafuta Wafadhili wa Kuendesha semina kwa Wafanyakazi na watumishi, lakini pia kuanzisha Mradi wa pamoja wa Kulinda haki za watoto wa kike katika masuala ya mimba za utotoni, ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia n.k ambapo mradi huu unatarajiwa pia kulishirikisha Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la jinsia.

Itakumbukwa pia KADETFU chini ya ufadhili wa Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), wametekeleza Mradi wa Ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa Jamii (UUJ) katika sekta ya Elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, lengo hasa likiwa ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao, mradi ulioanza Julai hadi Desemba 2018.
 Mkurugenzi wa Shirika la KADETFU  Bwana. Yusto Muchuruza na Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Bukoba Mheshimiwa Murshidi Ngeze, wakikabidhiana Mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja kati ya Kadetfu na Halmashauri hiyo Januari 30, 2018 katika Ukumbi wa Chemba.
 Bwana Yusto Mchuruza Mkurugenzi wa KADETFU akitoa maelezo machache kabla ya Kukabidhiana mkataba kati ya KADETFU na Halmashauri ya Bukoba wa kushirikiana kufanya Shughuli mbalimbali kwenye Halmashauri hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Ufatiliaji wa uwajibikaji  wa watumishi wa umma, wakizungumza na Mkuu wa shule ya Msingi ya Ntoma iliyopo Kata Kanyangereko Wilayani Bukoba, juu ya Matumizi ya fedha za Shule hiyo.
 Afsa Mipango wa Wilaya ya Bukoba Bwana Julian Tarimo akitoa semina elekezi kwa wafanyakazi wa KADETFU katika maana ya ushirikiano uliopo kati ya pande zote mbili.




Comments

Popular posts from this blog