'Birthday' ya Dada Yamtesa Neymar Kwa Miaka Mitano



Baada ya siku kadhaa kupita tangu nyota wa PSG Neymar Jr alipotiwe kuumia kifundo cha mguu, leo imeweka wazi kuwa winga huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10.


Neymar akiwa na dada yake Rafaella

Taarifa za kuumia kwa Neymar zimegubikwa na utata hususani kuelekea Februari 11, ambayo huwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa dada yake Rafaella Santos na hawajawahi kukosa kuungana na dada yake huyo kwenye siku hiyo tangu atue kwenye soka la Ulaya mwaka 2013.

Neymar mwenye miaka 26, sasa amekosa michezo kadhaa ya mwezi wa pili kwa miaka mitano mfululizo ambapo huwa anaumia mwishoni wa Januari au mwanzoni mwa Februari.

Msimu wa 2014/15 akiwa Barcelona Neymar alikosa mchezo katika tarehe za siku ya kuzaliwa za dada yake kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu na alisafiri hadi Brazil kujumuika na dada yake.

Msimu wa 2015/16 akiwa hapo hapo Barcelona Neymar alikosa michezo miwili ya mwezi Februari ambapo pia ilikuwa ni kutokana na kadi nyekundu pia alihudhuria siku ya kuzaliwa ya dada yake.



Alimaliza maisha ya Barcelona kwa kukosa michezo kadhaa ya mwezi Februari kutokana na Majeruhi ambapo pia alikwenda kutibiwa Brazil na kuhudhuria sherehe ya dada yake.

Akiwa PSG huu sasa ni msimu wake wa pili mfululizo akiwa majeruhi ndani ya mwezi Februari na amekuwa akitibiwa nchini Brazil na hivi sasa tayari yupo nchini humo na huenda pia akawepo kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa dada yake.

Neymar atakosa michezo yote miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya mtoani ambapo PSG itacheza na Manchester United.

Wosia wa mama Abdul, wagoma msiba kuagwa | East Africa Television
Muigizaji mkongwe nchini Salome Nonge (Mama Abdul) ameacha wosia kwa ndugu zake, ambao walikuwa wakimuuguza mpaka mauti yalipompata nyumbani kwake Mburahati jijini Dar es salaam.
EATV

Zahera na Aussems wote wasusia ubingwa | East Africa Television
Kocha wa Simba, Patrick Aussems ameungana na kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ambapo wote amesema makombe ya Mapinduzi Cup na SportPesa hayakuwa sehemu ya mipango yao.




from UDAKU SPECIAL BLOG

Comments

Popular posts from this blog