KESHO DROO YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA, ZAIDI SOMA HAPA

Hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya imekamilika jana kwa michezo miliwili kupigwa.

Mchezo wa mapema zaidi ulikuwa kati ya Besiktas ambayo iliikaribisha Bayern Munch vinara hawa wa ligi kuu nchini ujerumani.

Kwenye mchezo huo klabu ya Bayern Munch iliilaza mwenyeji Besiktas kwa jumla ya mabao matatu kwa moja na kutinga hatua ya nane bora kwa uwiano wa magoli nane.

Mchezo wa pili ulioanza majira ya saa nne usiku klabu ya Barcelona ya nchini Spain iliikaribisha Chelsea kutoka England.

Mnamo dakika ya tatu tu ya mchezo mshambuliaji wa Barcelona alionyesha ubora wake baada ya kuifungia goli la uongozi Barcelona.

Mchezo huu ulimaliza kwa Chelsea kuruhusu kipigo cha mabao matatu kwa sifuri Messi akiingia kambani mara mbili huku bao moja likifungwa na Dembele.

Lionel Messi sasa amefikisha magoli 100 katika Uefa champions league kwenye michezo 123 aliyocheza akimfunika Ronaldo ambaye alifikisha goli 100 katika michezo 137.

Jumla ya timu ambazo zimetinga hatua ya nane bora UEFA Champions League

1:Real Madrid
2:Liverpool
3:Manchester City
4:Sevilla
5:Bayern Munich
6:Barcelona Fc
7:Roma
8:Juventus

Droo ya kujua nani anakutana na nani itachezeshwa siku ya Ijumaa kesho.

Comments

Popular posts from this blog

Njia sahihi za kuachana na unywaji wa pombe