MATOKEO VPL LEO JUMAPILI DECEMBER 31-2017

Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo kwa michezo miwili katika raundi ya 12, ambapo mchezo wa kwanza ulizikutanisha Njombe Mji waliowakaribisha Singida United katika uwanja wa Sabasaba Njombe.

Mchezo hu ulianza majira ya saa 14:00 mchana na Singida United kufanikiwa kupata ushindi mnono wa goli 3-1, magoli ya Singida yamefungwa na Elinywesia Sumbi dakika ya 18, Shafiq Batambuze dakika ya 66 na Deus Kaseke dakika ya 82.

Goli pekee la Njombe Mji limefungwa na Awadh Salim kunako dakika ya 42.

Mchezo wa pili uliwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Young Africans na Mbao FC kutoka Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huu ulianza majira ya saa 16:00 jioni na Mbao Fc kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0, magoli ya Mbao yamefungwa na Habib Kiyombo katika dakika ya 53 na 68.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho katika kukamilisha raundi ya 12 msimu wa 2017-2018.

Comments

Popular posts from this blog