TAARIFA YA DAKTARI WA YANGA KAMA KAMSOKO ATACHEZA LEO DHIDI YA MTIBWA SUGAR
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga leo ni kuhusu taarifa za majeruhi kuelekea mechi yao na Mtibwa Sugar 16:00 jioni katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa Daktari wa timu ya hiyo Edward Bavu amethibitisha kuwa wachezaji wote wanaweza wakatumika kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa isipokuwa Amis Tambwe na Papy Tshishimbi mwenye kadi 3 za njano.
Ten anasema Dakatari huyo amemthibitishia Kuwa Amis Tambwe na Tshishimbi ndiyo wachezaji watakaoukosa mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar, huku Tabwe akiwa amerejea kutoka katika majeraha siku za hivi karibuni kwa sababu hiyo bado hajawa sawa kwa asilimia 100.
Jana tulikuwa na taarifa za uwezekano wa kumkosa Thaban Kamsoko katika mchezo wa leo kutokana na kuwa na jeraha la goti sasa ni rasmi Kamsoko yupo fiti kwa asilimia 100. KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU KWA KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI.
WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII
Comments
Post a Comment