MATOKEO MECHI ZA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA SEPTEMBER 30-2017

Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea leo kwa mzunguko wa tano, mwendelezo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018 kwa Jumla ya viwanja 7 kuwaka moto.

 1:Katika Uwanja wa Uhuru tumeshuhudia Vinara wa Ligi Mtibwa Sugar wakilazimisha sare ya bila kufungana na Mabingwa wa Ligi 2016-2017 Young African.

Matokeo katika Viwanja vingine 
2:Azam Fc imelazimishana sare ya goli 1-1 huku goli la Singida United likifungwa na Danny Usenginmana na la Azam Fc limefunga na Pauo Peter.

3:Mbao Fc ya Mwanza yenyewe imepata sare nyingine baada ya ile ya Simba kufungana 2-2 pale CCM Kirumba leo imepata sare nyingine kutoka kwa Maafande wa Tanzania, Tanzania Prisons, goli la Mbao Limefungwa na Kotecha huku la Tanzania Persons likifungwa na Mpepo.

4:Mwadui Fc nayo imetoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Mbeya City, magoli ya Mwadui yamefungwa na Benard yote mawili na ya Mbeya City yamefungwa na Mohammed Samatta na Mkopi.

5:Ndanda Fc imepata ushindi wa goli 2-1 ikiwa nyumbani ilipoikaribisha Lipuli Fc, magoli ya Ndanda yamefungwa na Kelvin pamoja na Elias huku la Njombe akijifunga Asante Kwasi.

6:Ruvu Shooting imeendeleza wimbi la droo baada ya leo kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Njombe Mji, goli la Ruvu Shooting limefungwa na Mcha huku la Njombe Mji likifungwa na Gwamaka.

7:Majimaji imetoka sare ya bila kufungana na wanankurukumbi wa Misenyi, Kagera Sugar, kwa matokeo haya Kagera Sugar inaendeleza rekodi mbaya ya kutofunga mechi hata moja toka Ligi hii ianze ikiwa na pointi 2 baada ya kutoa sare na Ruvu Shooting na sare ya leo dhidi ya Majimaji.

Ligi hiyo itaendele tena kesho kwa mechi moja kati ya Stand United ya mkoani Shinyanga dhidi ya Simba Sc ya Jijini Dar es salaam, katika Uwanja wa Kambarage-Shinyanga.

KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU KWA KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI.
KAMA UNA PICHA, VIDEO AU HABARI ZINAZOHUSU MICHEZO AU MATANGAZO WASILIANA NAMI KWA NAMBA,0756658100, email-erickkaberwa2015@gmail.com.

WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Comments

Popular posts from this blog