HUYU HAPA KOCHA WA MUDA FC BUYERN MUNICH
Baada ya kocha mkuu Buyern Munich Carlos Ancelotti kutfutwa kazi Uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa timu kwa muda Willy Sagnol ambaye pia matokeo yanaweza kuamua nafasi yake.
Pamoja na kutumia muda wake mwingi wa soka katika nchi ya Ujerumani lakini Sagnol sio Mjerumani, Sagnol ni raia wa Ufaransa na alizaliwa Ufaransa katika jiji la Ettiene, hiyo ilikuwa mwaka 1977.
Sagnol katikati ya mwaka 2002 na 2009 aliitumikia Bayern Munich katika michezo zaidi ya 180 huku akifanikiwa kubeba makombe 10 na klabu hiyo, ni wazi kwamba anaijua vyema Bayern Munich na anajua utamaduni wa klabu hiyo.
Mwaka 2008 Sagnol aliingia katika vichwa vya habari nchini Ujerumani baada ya ugomvi mkubwa kati yake na kocha wa Bayern Munich kipindi hicho Ottmar Hitzfield ugomvi uliopelekea Sagnol kutoswa katika kikosi cha Bayern kilichosafiri kwenda kucheza na St Petersburg.
Sagnol mwaka 2000 pia aliingia katika mzozo na klabu ya Ufaransa ya Monaco kuhusu maslahi baada ya Sagnol kudai ya kwamba Monaco walikuwa wakimlipa kiasi kidogo sana cha pesa na kumuona mjinga kwa kuwa alikuwa na umri mdogo kitu kilichomfanya kuachana nao.
Sagnol ambaye kwa mashabiki wa Bayern anafahamika kama “The God Of Cross” aliwahi kuifundisha klabu ya Ligue 1 ya Bordeaux lakini pia amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 21 na baada ya uwepo wake katila benchi la ufundi la Bayern Munich sasa anakwenda kuwa kocha mkuu. KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU KWA KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI.KAMA UNA PICHA, VIDEO AU HABARI ZINAZOHUSU MICHEZO AU MATANGAZO WASILIANA NAMI KWA NAMBA,0756658100, email-erickkaberwa2015@gmail.com.
WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII
Comments
Post a Comment