Usajili: Athuman Idd Chuji huyu hapa arejea tena Ligi Kuu.

Klabu Ya Ndanda Fc ya Mtwara imefanikiwa kuinasa saini ya Kiungo wa Zamani wa Yanga Athumani Iddi ‘Chuji’

Chuji amejiunga na Ndanda Fc kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea klabu hiyo kwa msimu wa 2017/2018.

Juhudi zake za kurejea Ligi Kuu Bara zilionyesha kutokuwa na mafanikio hata alipojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo licha ya kukaa misimu miwili, hakupata nafasi ya kucheza.

Baada ya hapo, Chuji aliamua kujiweka kando mwa ligi hiyo na hivi karibuni aliibuka na kufanya vizuri katika michuano ya Ndondo FC.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPO CHINI ILI UWE WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU
NA KWA HABARI YOYOTE YA MICHEZO USISITE KUTUTUMIA WHATSAPP NO:0756658100 TOA MAONI YAKO HAPA USITUKANE.

Comments

Popular posts from this blog