TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO APRIL 30




MAN UTD YAMTENGEA DAU DEULOFEU

Manchester United wanajipanga kutoa dau nono kumsajli Gerard Deulofeu msimu wa majira ya joto, kwa mujibu wa Don Balon .
Winga huyo anatumika kwa mkopo Milan akitokea Everton, klabu yake mama na iliyomtwaa kwa mkopo zote zinahita huduma yake msimu ujao.
Klabu ya zamani ya Deulofeu, Barcelona ina kipengele kinachoiruhusu kumnunua winga huyo wa Kihispania kwa euro milioni 12.

TALISCA ALIYEKO KWENYE RADA ZA UNITED ANAUZWA


Mchezaji ambayeManchester United inamuwinda, Anderson Talisca anatarajia kuwekwa sokoni majira ya joto, na thamani yake ni paundi milioni 21 Daily Star .
Kiungo huyo mshambuliaji wa Benfica kwa sasa anakipiga kwa mkopo Besiktas, lakini Jorge Mendes ameahidi kumruhusu mteja wake kuondoka Ureno dirisha la usajili litakapofunguliwa.

THEO HERNANDEZ ANAKARIBIA KUTUA BARCA

Barcelona wanakaribia kumsajili Theo Hernandez kutoka Atletico Madrid kwa mujibu wa Sport.
Real Madrid pia walikuwa wanataka kuinasa saini ya Hernandez kutoka kwa mahasimu wao, lakini Barca imejipanga vema kutoa euro milioni 24 zinazohitajika kumnunua.

LIVERPOOL YAMTENGEA ISCO DAU
Liverpool wanajipanga kumsajili kiungo mahiri wa Real Madrid majira ya joto, kulingana na habari za Don Balon .
Jurgen Klopp anataka kupata mbadala wa Philippe Coutinho anayefukuziwa kwa kasi na Barcelona, na anaamini Muhispania huyo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo.
Isco anaonekana kuwa tayari kusani mkataba mpya kubaki Santiago Bernabeu, lakini anaweza kuigeukia Liverpool pia.

HART YUPO TAYARI KUTUA MAN UNITED
Joe Hart yupo tayari kujiunga na mahasimu wakubwa wa Manchester City, Manchester United dirisha la uhamisho wa majira ya joto litakapofunguliwa Sun .
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akitumika kwa mkopo Torino baada ya kushindwa kuoneysha ushawishi kwa kocha mppya Pep Guardiola, na iwapo De Gea atauzwa, basi atakuwa na nafasi kubwa kutua Old Trafford.

ARSENAL YAMTOLEA UDENDA BENDER
Arsenal kwa karibu sana inamfuatilia mchezaji wa Borussia Dortmund Sven Bender kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .
Washika Mtutu hao wamelaumiwa kwa kupungukiwa ustahimilivu eneo la kati wakiwa dimbani, Bender anaonekana kuwa mtu sahihi kwa shughuli hiyo kama kiungo au beki wa kati.

NEYMAR ANATARAJIA KUTUA UNITED
Gazeti la Daily Record limeripoti kuwa Neymar anatarajia Manchester United itanunua mkataba wake wa euro milioni 200 kutoka Barcelona.
Makala hiyo inadai kuwa kuelekea msimu wake wa pili Old Trafford, Jose Mourinho anafikiria namna ya kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic na yupo tayari kufanya kila namna kumpata nyota huyo wa Kibrazili.

JAMES KUVAA JEZI #10 YA ROONEY
James Rodriguez anatarajia kutua Manchester United msimu wa majira ya joto na anatazamia kuvaa jezi nambari 10 ya Wayne Rooney, limedai Don Balon .
Chanzo hicho cha Hispania kimdai kuwa Jose Mourinho anafanya mpango wa kumsajili Mcolombia huyo na anaamini ni mbadala sahihi wa Rooney, ambaye anatarajiwa kuondoka Old Trafford mwisho wa msimu

BARCA NA MADRID ZAMPGANIA SILVA
Barcelona wanaamini wataizidi nguvu Real Madrid katika vita ya kumsajili nyota wa Monaco, Bernardo Silva, kwa mujibu wa Diario Gol .
Habari zinadai kuwa miamba hao wa Catalan wanahofu kuwa mahasimu wao wa Clasico wanaweza kuwazidi ujanja kwa sababu ya uhusiano wa karibu na Jorge Mendes - anayemwakilisha Cristiano Ronaldo. Anaweza kuwapendelea Los Blancos kwa saini ya nyota huyo.

MAN UTD YAZUNGUMZA NA OBLAK
Manchester United wameanza mazungumzo na wawakilishi wa kipa wa Atletico Madrid Jan Oblak, kwa mujibu wa Manchester Evening News .
Mashetani hao Wekundu wana hofu ya kumpoteza David de Gea kwa Real Madrid majira ya joto, na wanataka kupata mbadala wake haraka iwezekanavyo.
Na wawakilishi wa wachezaji wa kimataifa wa Slovenia Oblak wamekuwa mjini Manchester kuangalia namna ya kukamilisha dili hilo.

MAN UTD YAONGOZA MBIO ZA AURIER
Manchester United wanaongoza katika mbio za kuiwania saini ya beki matata wa PSG Serge Aurier, limeripoti The Sun .
Beki huyo wa ameripotiwa kufanya mazungumzo na Jose Mourinho na United wameipiku Manchester City na Barcelona katika mbio za kumsajili mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 20.
PSG wamempa dili jipya mchezaji huyo kubaki Ligue 1, lakini yupo tayari kuondoka kwenye klabu hiyo.

DONNARUMMA KUSAINI MKATABA MPYA MILAN
Kipa matata wa AC Milan Gianluigi Donnarumma anatarajiwa kupewa mkataba mpya zikiwa ni jitihada za kuizuia Manchester United kumsajili, kwa mujibu wa La Repubblica .
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 18 amejiimarisha kama moja ya makipa bora katika soka la Ulaya tangu alipopata fursa ya kucheza kikosi cha kwanza kwenyt klabu hiyo ya Serie A, Jose Mourinho akiwa katika harakati za kuipata saini yake kama mrithi wa David De Gea Old Trafford.

JAMES ANATAKA KUTUA MAN UTD
James Rodriguez amekosa maelewano mazuri na Zinedine Zidane na anataka kuondoka Real Madrid kwa mujibu wa Don Balon .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kikosi cha kwanza Bernabeu na anatamani kujiunga na Old Trafford.

MADRID YATENGA DAU NONO KWA AJILI YA MBAPPE
Real Madrid wapo tayari kutoa dau la euro milioni 100 kwa ajili ya kinda matata wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa L'Equipe .
Zinedine Zidane ni shabiki mkubwa wa Mfaransa mwenzake na yupo tayari kuvunja benki kuwashinda miamba wengine wa Ulaya wanaoitaka saini ya nyota huyo.

MAN UTD YAMTAKA GRIEZMANN & BELOTTI
Manchester United inajipanga kutumia paundi milioni 170 majira ya joto kuwasajili Antoine Griezmann na Andrea Belotti, kwa mujibu wa Independent .
Mashetani Wekundu wanavyo vyanzo vya fedha kukamilisha usajili wa wachezaji hao wawili lakini pia kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic na Wayne Rooney kutafanya mchakato huo kuwa rahisi.

DE GEA RUKSA KUONDOKA UNITED
Jose Mourinho amesema hawezi kumzuia mchezaji yeyote anayetaka kuondoka Manchester United majira ya joto, kwa mujibu wa Marca.
Kocha huyo amewaambia wachezaji wanaohusishwa na tetesi zinazowazunguka kama David De Gea, Zlatan Ibrahimovic na Ander Herrera kwamba atawauza kama wanataka kuondoka.

ZLATAN AKUBALI HABARI YAKE IMEISHA UNITED
Zlatan Ibrahimovic amekubali kwamba habari yake imeishia Manchester United baada ya kupata majeraha ya ligamenti kwa mujibu wa the Daily Mirror .
Veterani huyo anayetimiza miaka 36 mwezi Oktoba atakuwa akifikiria kutimkia MLS, kwa lengo la kurejea dimbani miezi tisa ijayo hadi mwaka.

LOW KUMRITHI ZIDANE
Chanzo kimoja cha Hispania AS kimedai kuwa Zinedine Zidane atatupiwa virago mwisho wa msimu huu iwapo atashindwa kuipatia klabu ubingwa wowote.
Ripoti zinadai kuwa Zizzou ameanza kuwa kwenye wakati mgumu kufuatia kipigo cha Jumapili dhidi ya Barcelona na inaaminika kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani anafuatiliwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mfaransa huyo atakapotimuliwa.

MAN CITY WANAMTAKA AURIER WA PSG
Manchester City imeungana na Manchester United na Barcelona kufukuzia saini ya beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, kwa mujibu wa Daily Mail .
Miamba hao wa Etihad wanaweza kupata wakati mgumu kwenye mazungumza kwani PSG licha ya matatizo ya kinidhamu ya mchezaji huyo wanajiandaaThe Citizens could find negotiations difficult, however, as PSG – despite the Ivory Coast international's disciplinary problems – are said to be preparing a new contract for the 24-year-old.

INTER YAMPA SIMEONE SIKU 20
Inter wametenga dau kumleta Diego Simeone San Siro msimu ujao, lakini wamempa bosi huyo wa Atletico siku 20 tu kuamua, kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport .
Ripoti zinadai kuwa ni ofa ya mkataba wa miaka mitano, na Mwargentina huyo atalipwa euro milioni 11 kwa msimu kama atakubali kutua Italia.

CHELSEA YAMTOLEA OFA BERNARDESCHI
Chelsea imepiga hatua katika harakati zao kumfukuzia winga wa Fiorentina Federico Bernardeschi, kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga magoli 13 msimu huu na ametengewa ofa ya paundi milioni 4.2 kwa msimu baada ya kodi ili kutua Darajani.

ARSENAL YAMWANDALIA DAU FORSBERG
Arsenal wanaandaa dau la paundi milioni 20 kwa ajili ya mshambulizi wa RB Leipzig Emil Forsberg, kwa mujibu wa The Sun .
Washika Mtutu hao wamevutiwa na kazi anayoifanya kijana huyo kwenye Ligi ya Ujerumani, Bundesliga na wanataka kumsajili sambamba na Sead Kolasinac ambaye ameshakubali kutua London.

CHELSEA YAWANYATIA LUKAKU & VAN DIJK
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amewapa kipaumbele Romelu Lukaku na Virgil van Dijk kuelekea uhamisho wa majira ya joto kwa, mujibu wa Daily Mirror .
Mshambulizi huyo wa Everton na beki wa Southampton wanaweza kugharimu paundi milioni 120, lakini Conte anataka kukiimarisha kikosi chake licha ya nafasi kubwa kutwaa ubingwa Ligi ya Uingereza waliyo nayo msimu huu.

REAL YAJIPANGA KUMSAJILI DYBALA
Real Madrid wapo tayari kuipatia Juventus wachezaji wawili ili kuipata saini ya Paulo Dybala uhamisho wa majira ya joto kwa mujibu wa Don Balon .
Zinedine Zidane yu tayari kuwatoa James Rodriguez na Alvaro Morata kwa miamaba hao wa Serie A ili kuipata saini ya Mwargentina huyo.

MAN UTD YAMUULIZIA MORATA
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefanya mazungumzo na viongozi wa Real Madrid kuhusu uwezekano wa kumpata mshambulizi Alvaro Morata, kimeripoti Don Balon .
Mashetani Wekundu wanajiandaa na maisha baada ya Zlatan Ibrahimovic, baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Sweden kupata majeraha yatakayomkosesha muda uliobakia wa msimu.

CITY YAINGIA MBIO ZA KUMSAJILI GRIEZMANN
Manchester City imeingia kwenye mbio za kutaka kumleta mshambulizi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann kwenye ligi ya Uingereza, limeripoti Daily Mail .
Manchester United na Chelsea zote zinaitamani huduma ya Mfaransa huyo ambaye anaweza kugharimu kiasi cha £75 millioni.

ARSENAL YATAFUTA MRITHI WA OZIL
Arsenal wanakaribia kuinasa saini ya mchezaji wa Barcelona Arda Turan kwa mujibu wa CNN Turk kupitia The Sun .
Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid ameshindwa kupata namba kikosi cha kwanza Camp Nou na Gunners wanataka kumsajli kuchukua nafasi ya Mesut Ozili ambaye ana kila dalili ya kuondoka Emirates majira ya joto.

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMPATA ROBERTSON
Liverpool wanakaribia kumpata beki wa Hull City Andrew Robertson kwa kitita cha paundi milioni 8 kwa mujibu wa Daily Mail .
Jurgen Klopp anataka kusajili beki wa kushoto na anaamini mchezaji huyo wa kimataifa wa Schotland atatatua tatizo lake kwa bei rahisi.

OFA YA ASENSIO YA €50M YAKATALIWA
Liverpool walitoa ofa ya euro milioni 50 sawa na paundi milioni 42 kwa ajili ya nyota wa Real Madrid Marco Asensio ambayo imekataliwa kwa mujibu wa AS .
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21 amekuwa mtu muhimu kwenye mipango ya Zidane kwenye kikosi cha Real Madrid.

PEREZ ANATAKA KURUDI DEPORTIVO
Lucas Perez na Deportivo La Coruna wamefanya mawasiliano kuzungumzia uwezekano wa mchezaji huyo kurejea kwenye klabu yake ya zamani baada ya kuchemka Arsenal kwa mujibu wa La Voz de Galicia .

RONALDO AMTAKA LEWANDOWSKI REAL
Cristiano Ronaldo anataka kumwonaRobert Lewandowski akijiunga na klabu ya Real Madrid msimu ujao wa majira ya joto kwa mujibu wa AS .
Inaaminika Mreno huyo amemwambia Robert Lewandowski kwamba anayo nafasi yake kwenye kikosi cha Real Madrid.

CITY YATENGA £50M KUMSAJILI BONUCCI
Manchester City watalazimika kulipa kiasi cha paundi milioni 50 kumpata beki wa Juventus Leonardo Bonucc, limeripoti Daily Telegraph .
Bei hiyo itamfanya Muitaliano huyo kuwa beki ghali zaidi katika historia, lakini City wapo tayari kutumia fedha za kutosha kufanya usajli ili kuwa imara zaidi ya Chelsea na Manchester United.

CONTE AJIPANGA KUMSAJILI MBAPPE
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumwongeza kinda wa Monaco Kylian Mbappe katika orodha ya wachezaji anaowataka majira ya joto kwa mujibu wa RMC .

Mabao ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 yameipaisha Monaco hadi hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya, na Conte yupo tayari kuishawishi klabu hiyo ya Ligue 1 kumwachilia kinda huyo





TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
For Booking>>> 
CALL>>>
Vodacom: +255756658100
 Tigo: +255655658100
JIUNGE NAMI KUPITIA

Comments

Popular posts from this blog