MWAMBUSI: YANGA TUKO FITI KUIVAA MBAO FC



Kocha msaidizi wa Yanga SC, Juma Mwambusi amesema wapo tayari kuwavaa Mbao FC na wamewaomba mashabiki wa klabu hiyo waliopo Mwanza na mikoa ya jirani wafike kuwapa sapoti na kushuhudia mpira safi toka kwa vijana wao.
Mwalimu huyo amesema hawezi kuidharau Mbao FC kwani ni timu nzuri na yenye ushindani mkubwa hivyo wanahitaji kucheza kwa tahadhari na umakini mkubwa ili kuibuka na ushindi wa pointi zote tatu.
"Tumejiandaa vyema na tunamshukuru Mungu tumemaliza mazoezi yetu salama na tupo tayari sasa kuwavaa Mbao Fc, kikubwa mashabiki wetu wa Mwanza na mikoa ya karibu wafike kwa wingi waje kuona mpira safi kabisa toka kwa vijana wao na tunaamini ata Mbao nao wataonyesha mpira mzuri na waupinzani mkubwa"-Juma Mwamusi Mwalimu Yanga SC.

Aidha, katika mchezo huu wa nusu fainali ya Kombe la FA utakaochezwa leo saa kumi jioni katika viwanja vya CCM Karumba, Jijini Mwanza mshindi wake atakutana kwenye fainali na Simba SC iliyoshinda goli 1:0 dhidi ya Azam FC jana.


TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
For Booking>>> 
CALL>>>
Vodacom: +255756658100
 Tigo: +255655658100
JIUNGE NAMI KUPITIA

Comments

Popular posts from this blog