JUAN MATA KUREJEA DIMBANI LEO MANCHESTER UNITED IKIIVAA SWANSEA CITY


Baada ya kuuguza majeraha kwa muda wa wiki nne, Juan Mata anatarajiwa kurejea dimbani kwa mechi ya Man United dhidi ya Swansea Jumapili
Juan Mata yu tayari kurejea kwenye kikosi cha Manchester United kitakachoikabili Swansea ikiwa ni wiki nne tu tangu alipopata majeraha.
Antonio Valencia ndiye aliyedokeza juu ya uzima wa Mata kwenye chapisho la kwenye Instagram Jumamosi jioni na Muhispania huyo alinaswa akiwaonyesha ishara ya dole gumba wapiga picha wa M.E.N akiwasili na wachezaji wenzake Lowry Hotel.
Wapiga picha walimuuliza Mata kabla ya mazoezi ni lini anatarajia kurejea dimbani naye aliwajibu: "Muda mchache sana nitakuwa nimerejea."
Meneja wa United Jose Mourinho alieleza Alhamisi kwamba anamtarajia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kucheza tena msimu huu.
"Nadhani Mata ndiye atakayekuwa wa kwanza kupona," alisema Mourinho. "Jambo litakalotupa chaguo jingine kwenye safu ya mashambulizi, lakini kwa kweli tunachohitaji zaidi ni mmoja wa mabeki wetu wa kati arudi."
Mata alidokeza kwenye blogu yake Jumatatu kwamba atarejea kwenye kikosi cha United ndani ya muda mchache.
"Najisikia vizuri zaidi sasa na natumai kurejea kikosini haraka, kuisaidia timu kwenye mechi za mwisho za msimu," alisema Mata. "Natarajia hivyo kwa sababu hilo ndilo nilitakalo; kuwa tayar muda wote kuisaidia timu kadiri ya uwezo wangu, nje na ndani ya dimba."

Awali Mourinho alisema anamtarajia Mata kurejea dimbani mwishoni mwa mwezi Mei na Chris Smalling na Phil Jones katikati ya mwezi Mei.



TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
For Booking>>> 
CALL>>>
Vodacom: +255756658100
 Tigo: +255655658100
JIUNGE NAMI KUPITIA

Comments

Popular posts from this blog