MATATIZO MATANO YA ARSENAL NA WACHEZAJI WAKE

Ligi ya Mabingwa UEFA ni miongoni mwa michuano bora, ukiwa na udhaifu wowote utabainishwa na timu bora kama yaliyowakuta Barca na Arsenal

1:Tatizo La Kwanza: Coquelin

Francis Coquelin alidhalilishwa na Eden Hazard aliyempita kirahisi na kuifungia Chelsea goli dhidi ya Arsenal. Mechi ya jana, pamoja na mapungufu yake lukuki msimu huu amewakumbusha wengi kwamba miaka mitatu ilyopita alikuwa kwenye benchi la Charlton.
Ubongo wake umezubaa kiasi cha kuigharimu Arsenal. Anacheza chini ya kiwango, ameishiwa mbinu za ukabaji na hana ubunifu.
Kama kuna jambo moja ambalo Wenger alipaswa kuiambia timu yake - ni hili "Msimruhusu Robbern kuutumia mguu wake wa kushoto kupiga mashuti." Ilichukua dakika kumi tu. Jamaa akatikisa nyavu za Arsenal kwa bonge la shuti. Hapa pia tutapata tatizo namba mbili.

2:Tatizo Namba Mbili: Ozil

Hakuna ubishi kwamba Mesut Ozil ni mchezaji mwenye maujuzi na weledi wa hali ya juu, lakini kwenye kipengele cha ukabaji ni tatizo.
Si kwenye kukaba tu lakini Ozil hana nguvu, si shupavu.

3:Tatizo la Tatu: Jazba za Sanchez

Arsenal wanatamani sana kumwongeza mkataba Alexis Sanchez, ambaye anaonekana kukerwa na wachezaji wenzake, iwe ni Olivier Giroud anayesherekea goli la kusawazisha dhidi ya Bournemouth au wachezaji wenzake kushindwa kucheza kwa jitihada dhidi ya Bayern kipindi cha kwanza.

4:Tatizo la Nne: Mawasiliano Duni baina ya wachezaji
Namna goli la pili la Bayern lilivyopatikana. Lahm anakimbia mbele kutengeneza 2 dhidi ya 1 akiwa na Robben dhidi ya Kieran Gibbs. Ni mapema mno kwa mtu kama Lahm kustaafu kwa kiwango alichofanya katika umri wa miaka 33 ukilinganisha na Alex Iwobi mwenye miaka 20.
Bayern walipokuwa na mpira, Alonso alipewa nafasi kubwa mno na Arsenal walishindwa kumzuia kupiga pasi.

5:Tatizo la Tano: Ukabaji dhaifu na Kutofanya maamuzi sahihi

Arsenal walikuwa na nafasi nne za kuondosha mpira kwenye eneo la hatari Bayern walipofunga goli la nne, wakati Thiago alipobaki huru ndani ya boksi kwa kipindi chote. Lilikuwa jukumu la Mesut Ozil.
Hitimisho
Arsene Wenger amefanya makubwa kwenye timu ya Arsenal siku za nyuma, lakini matatizo yanazidi kuongezeka. Wapo kwenye njia ya kutokea hatua ya 16-Bora michuano ya Uefa. Bodi ya Arsenal inajipima kama impe Mfaransa huyo mkataba mpya - Kiwango chao dhidi ya Bayern kilikuwa hovyo kupita maelezo.

Comments

Popular posts from this blog