SIMBA KUMSAJILI KIPA WA MEDEAMA ALIYEWABANIA YANGA

Kama Agyei atatua Simba, niwazi atakuwa chaguo la kwanza na kuendelea kumsotesha benchi kipa Manyika Peter ambaye bado hajaaminika na makocha wa timu hiyo
Vinara wa ligi ya Vodacom Simba ipo kwenye hatua za mwisho kuinasa saini ya kipa namba moja wa klabu ya Medeama na timu ya taifa ya
Ghana Daniel Agyei .
Msemaji wa Simba Hajji Manara , ameiambia
Goal, uongozi wa juu ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu hiyo
Zacharia Hans Poppe, yupo nchini Ghana kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa Medeama ili kumsajili mchezaji huyo.
“Moja ya mapungufu yetu kwenye mzunguko wa kwanza ilikuwa ni kipa, hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya kocha kwaiyo kama uongozi tumeona nivyema tukalitilia mkazo na kuhakikisha tunalikamilisha haraka iwezekanavyo ili kuweze kutwaa ubingwa msimu huu,”amesema Manara.
Kiongozi huyo amesema wamemchagua Agyei, kwasababu wamevutiwa na kiwango chake alichokionyesha kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na wanaimani ndiyo chaguo halisi kwao kuziba nafasi ya Vicent Angban raia wa Ivory Coast .
Soma Pia: Omog Siri ya mafanikio Simba
Manara amesema awali walimpa jukumu hilo kocha wao Joseph Omog , lakini baada ya kukosa muda wa kutosha kocha huyo alilirudisha swala hilo kwa uongozi na wao moja kwa moja wakamtazama nyanda huyo wa Medeama.
“Nikipa mzuri tulimuona kazi aliyoifanya walipocheza na Yanga hapa lakini hata kwenye michezo mingine ya hatua hiyo ya makundi na ilibaki kidogo kuipeleka nusu fainali timu yake baada ya kuzidiwa kwa mabao ya kufungwa kati yao na MO Bejaia,”amesema Manara.
Simba ilikuwa ikimtegemea zaidi Angban aliyedaka michezo yote 15 ya mzunguko wa kwanza na kufungwa mabao sita, lakini kocha Omog, amesema kipa huyo amekosa changamoto baada ya msaidizi wake Manyika Peter kushindwa kuonyesha juhudi.

Comments

Popular posts from this blog