Ronaldo atoa zaidi ya bilioni 9 kama rambirambi kwa timu ya Chipacoense


Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidi kutengeneza CV yake nzuri kwa jamii – amekuwa ni mmoja kati ya watu walioguswa na msiba mkubwa uliotokea kwenye familia ya soka duniani kutokana na ajali ya ndege iliyotokea usiku wa Jumatatu hii nchini Clombia iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Chipacoense na watu wengine.

Ronaldo ameamua kuchangia kiasi cha euro milioni tatu kwa timu hiyo kama mchango wake wa rambirambi ambazo ni zaidi ya bilioni 9 za kitanzania.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuchangia kwenye matatizo kama hayo kwani hata mwaka jana alichangia kiasi cha paundi milioni 5 kwa wananchi wa Nepal waliokumbwa na mafuriko.

Comments

Popular posts from this blog