MANCHESTER UNITED BADO INA NAFASI YA KUTWAA UBINGWA EPL:PEP GUARDIOLA
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anaamini kwamba Manchester United bado ipo kwenye mbio za kushinda ubingwa wa EPL, sambamba na Man City, Chelsea, Liverpool, Spurs na Arsenal. Katika mahojiano na Televisheni ya klabu alisema. “Ligi ya mwaka huu haitabiriki na utabiri ni vyema ukaanza kufanyika katika miezi miwili au mitatu ya mwisho.
Manchester City ambayo ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 30 sawa na Liverpool bado inampa matumaini ya ubingwa Guardiola ambaye ameeleza kufurahia nafasi hiyo kutokana na kuwa timu zilizo juu yake yaani Chelsea na Liverpool zimewekeza nguvu zaidi kwenye EPL kwakuwa hazishiriki michuano ya Ulaya huku timu yake ikiwa inashiriki UEFA.
Guardiola ameisifu Chelsea kwa mfumo wa kutupa kijembe kuwa umahiri wa Chelsea unatokana na kutupwa nje ya kombe la ligi, hivyo kusalia katika mashindano mawili tu ya ndani. Amesema “Chelsea inacheza mara moja kwa wiki. Ni rahisi kujiandaa vizuri, Kupona vizuri na kujiandaa kikamilifu kwaajili ya michezo ya wikiendi lakini upande wetu tunacheza Jumatano pamoja na Jumamosi kwenye wiki ya michezo ya Ulaya”.
Pep alimaliza kwa kuwatoa wasiwasi mashabiki wa United kuwa timu hiyo inayonolewa na mpinzani wake Jose Mourinho bado ina nafasi ya kufanya vizuri. “Manchester United ni timu ambayo ipo kwenye timu tano zinazoweza kutwaa ubingwa msimu wa 2016/17 kwasababu msimu bado sana na wachezaji watazoeana na timu itafanya vyema”, alimaliza Guardiola.

Comments
Post a Comment