Taliss-IST yachangia timu za Taifa za mchezo wa kuogelea
Waogeleaji wa timu ya Taliss-IST wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki katika mashindano maalum ya kuzichangia fedha timu za Taifa za mchezo wa kuogelea ili zishiriki katika mashindano ya Dunia. Dar es Salaam. Mabingwa wa mchezo wa kuogelea nchini, Taliss- IST ya Upanga imechangia kiasi cha Sh1.5 millioni kwa ajili ya timu za taifa za mchezo huo zinazojiandaa na mashindano ya Dunia mjini Gwangju, Korea Kusini na mashindano ya vijana ya dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Budapest, Hungary. Klabu hiyo iliwakilisha fedha hizo katika mashindano maalum yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert yaliyoandaliwa na Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA). Taliss-IST ilichangia fedha taslimu Sh1,225,000 na dola za Kimarekani 140 katika mashindano hayo maalum ambayo yalishirikisha waogeleaji wenye umri tofauti. Waogeleaji hao hao ni Mohameduwais Abullatif, Lara Steenkamp Aravind Raghavendran, Fallih Ahmed, Ahme...